• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema hakuna nchi yenye haki ya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2020-05-29 19:17:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo hapa Beijing amesema, uamuzi wa Bunge la Umma la China kupitisha sheria ya usalama wa taifa katika Hongkong ni mambo ya ndani ya China, na nchi yoyote haina haki ya kuingilia kati mambo hayo.

    Amesema China inahimiza nchi za nje kuheshimu mamlaka ya China, kuzuia kauli na vitendo vyake, kuacha kuingilia kati mambo ya Hongkong na mambo ya ndani ya China kwa njia yoyote.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani, Uingereza, Australia na Canada jana walitoa taarifa ya pamoja, wakisema Bunge la Umma la China kupitisha uamuzi wa kutunga sheria ya usalama wa taifa katika Hongkong ni kinyume cha wajibu wa kimataifa uliowekwa kwenye taarifa ya pamoja ya China na Uingereza, na kuharibu mwongozo wa "Nchi Moja Mifumo Miwili".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako