• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki watoa mwito wa mpango wa kuwaokoa kutokana na janga la Corona.

    (GMT+08:00) 2020-05-30 18:07:56

    Chama cha wafanyabiashara cha Afrika Mashariki kimesema kitafanya mazungumzo na serikali ili kuandaa mpango wa uokoaji kutokana na madhara ya virusi vya Corona, wakati wakisubiri uchumi wa nchi hizo kufunguliwa kwa ukamilifu.

    Mwenyekiti wa chama cha biashara, viwanda na kilimo cha Tanzania Bw. Paul Koyi, amesema chama chake kitakuja na sauti moja kuziambia serikali ni mpango gani ambao utakuwa mwafaka. Amesema wataandaa mapendekezo kwa serikali ambayo yatakuwa na mwongozo na mjadala kuhusu mahitaji ya kufufua uchumi kwa jumuiya ya wafanya biashara.

    Amesema suala la mpaka linaloziathiri Kenya, Uganda na Tanzania linatakiwa kushughulikiwa kwa haraka, na biashara kuendelea kwenye mpaka kunaweza kuchangia sana kupunguza hali ya sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako