• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kutekeleza ipasavyo malengo ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-05-30 18:08:55

    Mkutano mkuu wa Baraza la Serikali la China umesisitiza kuhusu utekelezaji wa sera na kazi za kutimiza malengo ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa mwaka 2020.

    Mkutano huo ulioendeshwa na waziri mkuu Bw. Li Keqiang umeeleza kuwa ripoti ya kazi ya serikali ambayo iliidhinishwa kwenye ufungaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China Alhamisi, iliweka malengo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kazi kuu kwa mwaka huu, ikihimiza serikali katika ngazi zote kutekeleza ipasavyo kazi na kukamilisha majukumu yao.

    Jumla ya majukumu makuu 51 yanayojikita katika maeneo 45 yamekabidhiwa kwa idara husika za Baraza la Serikali. Mkutano huo umezitaka serikali katika ngazi zote kutekeleza hatua za kutoa msaada kwa shughuli za kibiashara na kuchochea uhai kwenye masoko.

    Mkutano huo umesema utaratibu maalum utaanzishwa kuhakikisha kuwa fedha hizo zinakwenda moja kwa moja mashinani na kutumiwa kwa ufanisi, na kwamba kampuni zote na watu wenye mahitaji wanatakiwa kunufaika na sera hizo kihalisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako