• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi atoa salamu za Siku ya Watoto Duniani

    (GMT+08:00) 2020-05-31 18:40:38

    Rais Xi Jinping wa China amewapa salamu watoto wa makabila yote kote nchini kabla ya Siku ya Watoto Duniani inayoangukia kesho Juni, mosi.

    Rais Xi ametoa wito kwa watoto kusoma kwa bidii, kushikilia ndoto na imani zao, na kujenga miili na mawazo yenye nguvu ili kujiandaa kwa ajili ya kuchangia utimizaji wa Ndoto ya China ya kuhuisha taifa.

    Rais Xi amebainisha kuwa watoto wa nchi nzima wamejionea jinsi Wachina wanavyojitahidi kwa moyo mmoja kupambana na virusi vya Corona, na pia kuwashukuru watoto hao kwa kuunga mkono mapambano hayo kwa vitendo, jambo ambalo limeonesha moyo mzuri wa watoto wa China.

    Amezitaka kamati za Chama cha Kikomunisti cha China na serikali katika ngazi zote pamoja na jamii kuwahudumia watoto na kuandaa mazingira mazuri kwa ukuaji wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako