• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: KRU yaunda kamati ya kusikiliza maoni ya wadau juu ya msimu huu wa raga

    (GMT+08:00) 2020-06-01 08:54:16

    Shirikisho la Raga la Kenya (KRU) limeunda kamati ya watu sita ambao wametwikwa jukumu la kutathmini mapendekezo ya wadau kisha kuamua hatima ya kampeni za raga ya Kenya kwa msimu huu wa 2019-20. KRU itawakilishwa na mkurugenzi wa ratiba za mechi Hillary Itela kwa pamoja na wanachama wa bodi Moses Ndale na Peris Mukoko.

    Xavier Makuba wa KCB ataungana na wenzake Philip Jalango wa Kabras Sugar na George Mbaye wa Mwamba RFC kuwakilisha vikosi vya Ligi Kuu ya Kenya Cup. Kwa mujibu wa Oduor Gangla ambaye ni mwenyekiti wa KRU, kamati hiyo itatoa ripoti itakayotoa uamuzi wa ama kurejewa kwa kampeni za msimu huu au kufutiliwa mbali kwa msimu wote baada ya kuangalia hali mbalimbali. Iwapo mechi za raga zitarejewa baada ya serikali kuondoa marufuku iliyopo, basi hilo huenda likafanyika Julai kwa kuwa wachezaji watahitaji angalau kipindi cha kati ya wiki 6 na 8 kujiandaa. KRU ilibatilisha maamuzi yake ya kufutilia mbali msimu mzima wa 2019-20 baada ya presha kutoka kwa klabu za Kenya Cup zilizotishia kutafuta haki mahakamani kwa madai kwamba zilikuwa zimewekeza kiasi kikubwa cha fedha kwa minajili ya kampeni za msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako