• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini asema hatua za karantini zinapunguza kidhahiri kiwango cha maambukizi

    (GMT+08:00) 2020-06-01 09:03:19

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema hatua za karantini dhidi ya COVID-19 zimepunguza kidhahiri kiwango cha maambukizi nchini humo.

    Kwenye mazungumzo kwa njia ya video na Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini, rais Ramaphosa amesema kabla ya kuchukuliwa kwa hatua za karantini, idadi ya wagonjwa walioambukizwa  COVID-19 iliongezeka maradufu kwa siku mbili, lakini baada ya kuanza kutekelezwa kwa hatua hizo, muda wake umeongezeka hadi siku 15.

    Afrika Kusini iliweka ngazi ya tano ya zuio tarehe 27 mwezi Machi, baadaye ilipunguza zuio hilo hadi ngazi ya nne tarehe 1 mwezi Mei.

    Rais Ramaphosa amesema katika kipindi cha kupungua kwa ngazi ya zuio, yaani kipindi cha ngazi ya nne, muda wa kuongezeka maradufu kwa idadi ya maambukizi ulikuwa umefikia siku 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako