• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutunga sheria ya usalama wa taifa hakutaathiri hadhi ya Hong Kong kuwa kituo cha fedha cha kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-06-01 09:33:43

    Mkuu wa idara ya fedha ya serikali ya mkoa maalumu wa Hong Kong Bw. Paul Chan, amesema kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa ajili ya Hong Kong hakutaathiri mitaji kuingia na kutoka Hong Kong kwa uhuru, uendeshaji wa mfumo wa kiwango cha ubadilishaji wa fedha na hadhi ya Hong Kong kuwa kituo cha kifedha cha kimataifa.

    Bw. Chan ameyasema hayo kwenye Blog yake, akisema ingawa vikwazo vya Marekani vimesababisha masumbufu madogo kwa soko, lakini athari halisi ni ndogo kwa sasa.

    Bw. Chan amesisitiza kuwa Hong Kong haikubali udhibiti wa ubadilishaji wa fedha na kuhakikisha ubadilishaji wa dola ya Hong Kong na uhuru kwa mitaji kuingia na kutoka Hong Kong. Hii ni moja ya mambo yanayoamua hadhi ya Hong Kong kuwa kituo cha fedha cha kimataifa, na inahakikishwa kwenye sheria ya kimsingi ya Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako