• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Alexander Lacazette hana hamu ya kujiunga na Inter Milan

    (GMT+08:00) 2020-06-01 15:41:12

    Fowadi wa Arsenal, Alexander Lacazette anaripotiwa kutokuwa na hamu ya kuagana na Gunners na kuyoyomea Inter Milan. Lacazette amekuwa akihusishwa na kujiunga na Inter katika nafasi ya Lautaro Martinez ambaye anawindwa na Barcelona. Licha ya kutegemewa sana chini ya uongozi wa Arsene Wenger na Unai Emery, staa huyo wa zamani wa Lyon amepoteza kibali Emirates, huku Pierre-Emerick Aubameyang ndiye anapendelewa katika safu ya ushambulizi. Hali yake kwa sasa inasemekana kuwa inafuatiliwa na Inter ambao wanakumbana na hofu ya kumpoteza Lautaro kwa Barcelona. Tangu ajiunge na Gunners mnamo 2017, Mfaransa huyo ametingisha wavu mara 45.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako