• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu milioni 2 wa Hong Kong wasaini barua ya kuunga mkono sheria ya usalama wa taifa

    (GMT+08:00) 2020-06-01 19:04:01

    Karibu watu milioni 2.93 wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong wamesaini barua ya kuunga mkono sheria ya usalama wa taifa wakati wa kampeni ya siku nane katika mkoa huo.

    Mmoja wa waandaaji wa kampeni hiyo iliyofanywa na taasisi mpya inayoitwa Msimamo wa Pamoja Kuunga Mkono Sheria ya Usalama wa Taifa, Tam Yiu-chung amesema, kupitia barua hiyo wanatumaini kuonyesha uungaji mkono wa wakazi wa Hong Kong kwa uamuzi huo sahihi wa kujenga na kukamilisha mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa Mkoa wenye Utawala Maalum wa Hong Kong, ili kulinda usalama wa taifa.

    Taasisi hiyo ilikabidhi barua hiyo Ofisi ya mawasiliano ya serikali kuu ya China kwenye mkoa wa utawala maalum Hongkong mapema leo. Akipokea barua hiyo Mkurugenzi wa Ofisi hiyo Luo Huining amesema, idadi kubwa ya washiriki imeonyesha kidhahiri kuwa sheria ya usalama wa taifa imekubaliwa na ni hatua muhimu inayokabiliana na matarajio ya wakazi wa Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako