• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tahadhari lazima zichukuliwe baada ya utalii kurejea.

    (GMT+08:00) 2020-06-01 19:58:25

    Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, amesema utalii nchini lazima uendelee, licha ya kuwepo kwa janga la corona ambalo ni tishio duniani. Waziri anasema kwamba janga la virusi vya corona limeathiri kwa kiwango kikubwa ,sekta ya utalii nchini na hivyo kuathiri uchumi wa nchi pia.

    Hata hivyo, waziri huyo anasema kwa sasa dalili za kurejea kwa utaliikatika hali yake ya kawaida, zimeanza kuonekana baada ya watalii kuanza kuingia nchini. Akizungumza jijini Dar Es Salaam Jumamosi iliyopita, katika hafla ya kuzindua video maalum za kutambulisha utalii wa Tanzania duniani, waziri Kigwangalla alisema kwamba wizara yake imeweka mwongozo ambao unaelekeza hatua muhimu za kufanya, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, na kuwataka watalii na wananchi wanaohudumia watalii hao, kufuata mwongozo huo kujilinda dhidi ya hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.#

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako