• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar: Wakulima watakiwa kuwekeza kwenye viungo.

    (GMT+08:00) 2020-06-01 19:58:45

    Wizara ya biashara na viwanda imewataka wakulima kuwekeza katika kilimo cha mazao ya viungo ambayo soko lake lipo la uhakika ndani na nje ya nchi.

    Akizungumza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali, alisema mahitaji ya mazao ya viungo ni makubwa ulimwenguni, pamoja nay a ndani kwa viwanda viwili vya mafuta ya mimea pamoja na makonyo.

    Aliyataja mafuta ya mimea yanayotarajiwa kuzalishwa kuwa ni mkaratusi, mchaichai, mrehani na mdalasini.

    Waziri alisema kwamba Wizara ya Biashara na Viwanda , kazi kubwa wanayoifanya sasa, ni kuwahamasisha wananchi kuanzisha vikundi vya ushirika, na mabaraza ya vijana kuanzisha mashamba ya kilimo cha viungo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako