• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Ukusanyaji wa mapato ya serikali utapungua hadi dola bilioni 1.5.

    (GMT+08:00) 2020-06-01 19:59:04

    Ukusanyaji wa mapato ya serikali nchini Rwand umekisiwa kupungua hadi dola bilioni 1.5 kwa mwaka wa kifedha wa 2020/2021. Hii ni kutoka dola bilioni 1.6 iliyokuwa imekisiwa katika mwaka wa kifedha wa 2019/2020. Kupungua huku kunatokana na janga la virusi vya corona ambalo limelemaza uchumi wa taifa hilo tangu mwezi Machi mwaka huu.

    Sekta ambazo hutegemewa sana katika ukusanyaji wa ushur wa taifa kama vile hoteli, utalii , burudani na usafiri, zote zimeathirika pakubwa huku mauzo ya mazao ya shambani kwa mataifa ya nje na uchimbaji madini zote zikipata pigo pia.

    Kupungua kwa mapato ya serikali huenda kukaathiri miradi mingi ya kitaifa na kulazimu serikali kuchukuwa mkopo. Kulingana na Waziri wa Fedha w Rwanda Uzziel Ndagijimana, huenda serikali ikachukuwa mkopo wa dola milioni 837 kutoka nje ili kufanikisha bajeti yake ya mwaka wa kifedha wa 2020/2021.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako