• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vita dhidi ya virusi vya Corona barani Afrika inatatizwa na taarifa potofu na kutengwa

    (GMT+08:00) 2020-06-01 20:09:44

    Taasisi ya kimataifa ya hisani ya Save the Children imesema, vita dhidi ya virusi vya Corona barani Afrika inakwamishwa na kuenea kwa taarifa zisizo sahihi na kutengwa kwa waathirika na familia zao.

    Tathmini iliyofanywa na taasisi hiyo katika nchi mbalimbali za Afrika mwezi April imeonyesha kuwa, habari za kufikirika na zisizo za kweli kuhusu virusi hivyo zimeenea kwa kasi, hivyo kuleta ugumu katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona barani Afrika.

    Mkurugenzi wa Sera na Kampeni katika Taasisi hiyo tawi la Afrika Bw. Eric Hazard amesema, habari zisizo sahihi na za kufikirika kuhusu virusi hivyo zinaweza kuchelewesha kuwekwa na kutekelezwa kwa hatua zinazolenga kupunguza na kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo, ambavyo vinaweza kuenea kwa kasi, taratibu, na kwa kificho katika jamii.

    Tathmini hiyo iliyofanyika katika nchi za Somalia, Zambia na Tanzania imeashiria kutengwa kwa kiasi kikubwa kwa watu walioambukizwa na virusi vya Corona pamoja na wahudumu wa afya walio mstari wa mbele na jamii ya Waafrika wanaoishi nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako