• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yatoa dola milioni 2 kusaidia sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2020-06-02 08:43:05
    Nchini Kenya serikali imetoa dola milioni 20 ili kusaidia sekta ya utalii ambayo ni miongoni mwa zilizoathirika sana na janga la corona.

    Rais Uhuru Kenyatta akizungumza kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 57 tangu nchi hiyo ipate madaraka pia amesema hivi karibuni atatangaza hatua mpya za kuhusu sheria za ufungaji.

    Sherehe za madaraka za mwaka huu zimefanyika ikulu na ni wageni wachache tu walioalikwa.

    Hii ni kutokana na janga la corona.

    Gwaride la jeshi pia lilijumuisha maafisa wachache tu na wote waliofika walitakiwa kudumisha umbali wa angalau mita moja.

    Kwenye hotuba yake, rais Kenyatta amezungumzia mafanikio ya kiuchumi, miundo mbinu na utawala.

    Kenya inaadhimisha siku hii wakati walioambukizwawa virusi vya corona wakiwa ni zaidi ya 1400 na zaidi ya 60 kufariki.

    Taakwimu za wizara ya kazi na huduma za jamii zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 135,000 wamepoteza ajira kutokana na janga hilo.

    Miongoni mwa sekta zilizoathirika zaidi ni uchukuzi, utalii na uuzaji nje wa bidhaa.

    Jumatatu, rais Uhuru Kenyatta ametangaza afueni kwa sekta ya utalii.

    "Sekta ya Utalii imepata athari kubwa zaidi kutokana na ufungaji, kusimamishwa kwa safari za ndege kimataifa na kuanzishwa kwa ushauri wa kudumisha nafasi kati ya watu. Ili kusaidia sekta hii muhimu, na kulinda wadau wake dhidi ya hasara kubwa za kifedha, Serikali inatoa dola milioni 20 ili kusaidia hoteli na taasisi husika ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwalinda wafanyikazi wao"

    Kulingana na baraza la utalii na usafiri duniani WTTC sekta ya utalii nchini Kenya huchangia ajira kwa asilimia 10.

    Na mchango wake kwenye pato la kitaifa ni zaidi ya dola bilioni 6 kwa mwaka.

    Msaada uliotangazwa na serikali, umekaribishwa na wadau kwenye sekta hiyo kama vile Mohamed Hersi ambaye ni mwenyekiti wa chama cha utalii nchini Kenya.

    "Pesa hizo hasa zitasaidia kulipwa mishahara kwa wafanya kazi. Tutakutana tuangalie jinsi ya kugawanya hizo pesa kwa wale walioathrika"

    Kama nchi nyingi duniani serikali za Afrika pia zimeweka amri ya kutosafiri au kutotoka nje ili kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona, lakini sheria hiyo pia imekuwa na ugumu wa kudumishwa huku wananchi wakishindwa kupata uwiano kati ya kufanya biashara na kulinda afya zao.

    Tarehe 6 Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutangaza hatua zinazofuata baada ya kukamilika kwa kipindi cha siku 21 cha ufungaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako