• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yataka kuendelea kushirikiana na Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:10:17

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema shirika lake linapenda kuendelea kushirikiana na Marekani.

    Akizungumza na wanahabari amesema dunia nzima imenufaika na ushirikiano wa karibu wa serikali na watu wa Marekani kwa muda mrefu. Katika miongo kadhaa iliyopita, serikali na wananchi wa Marekani wametoa mchango mkubwa na kuleta athari chanya kwenye mambo ya afya duniani, na WHO inapenda ushirikiano huo uendelee.

    Tarehe 29 mwezi uliopita rais Donald Trump wa Marekani alisema nchi yake itakatisha uhusiano na WHO kutokana na shirika hilo kukataa kufanya mageuzi kama ilivyoagizwa na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako