• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaitaka Marekani kusimamisha vitendo vya kimabavu dhidi ya watu wake

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:30:02

    Msemaji wa serikali ya Iran Bw. Ali Rabiei amesema katika kila sehemu duniani, Marekani inaingilia ovyo mambo isiyoyapenda. Amesema Iran inafuatilia kwa karibu maendeleo ya hali ya maandamano nchini Marekani, na kuonyesha wasiwasi kuhusu hali ya ubaguzi wa rangi iliyopo sasa nchini humo na vitendo vya kimabavu vinavyotokana na hali hiyo. Anasema,

    "Marekani huwa inatumia kisingizio cha haki na uhuru kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine. Tukio hili linaonyesha kuwa Marekani haina haki ya kuzilaumu nchi nyingine juu ya haki za binadamu. Serikali ya Marekani badala ya kutumia muda wake kuharibu utulivu wa dunia, ingefuatilia mageuzi ya miundo na uhusiano wake wa kijamii, kuondoa hali isiyo na usawa wa uchumi na matabaka. Tunatumai serikali ya Marekani inaweza kujifunza kutokana na tukio hili, kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine ikiwemo Iran."

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Abbas Mousavi, amesema Iran inaunga mkono sera ya kuwepo kwa China moja, na inalaani vitendo vya kuingilia mambo ya ndani ya China. Pia imezitaka nchi za Magharibi kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi huru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako