• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump asema atapigania usalama wa wananchi wa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:40:03

    Rais Donald Trump wa Marekani jana alitoa hotuba kwenye Ikulu ya Marekani, siku ya nane baada ya mmarekani mweusi George Floyd kuuawa na polisi mzungu katika Jimbo la Minnesota.

    Shirika la habari la Marekani CNN limeripoti kuwa,rais Trump amesema serikali yake inahusika katika kutafuta haki kwa George Floyd, lakini pia anaona waporaji na maandamano ya kimabavu vimevuruga ufuatiliaji wa watu kwa lengo hili. Amesisitiza kuwa waathirika wakubwa zaidi ni wananchi wanaopenda amani ambao wanaishi kwenye mitaa maskini, na kwamba akiwa rais atapigania usalama wao.

    Kwa mujibu wa ripoti, wakati rais Trump alipotoa hotuba hiyo, sauti za waandamanaji zilisikika nje ya Ikulu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako