• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump aingia tena kwenye handaki la usalama chini ya Ikulu

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:40:30

    Maandamano ya kupinga kifo cha mmarekani mweusi George Floyd yanaendelea kutokea nchini Marekani. Shirika la habari la Marekani CNN limeripoti kuwa usiku wa tarehe 31 Mei, rais Donald Trump alikimbilia tena kwenye handaki la usalama chini ya Ikulu.

    Kabla ya hapo ofisa wa Ikulu na watekeleza sheria walieleza kuwa, usiku wa tarehe 29 rais Trump alihamishwa kwenye handaki hilo la usalama kwa muda wa karibu saa moja.

    CNN imeripoti kuwa kabla ya rais Trump kuingia tena kwenye handaki, maandamano yalisambaa kote Marekani, hata nje ya Ikulu. Tarehe 31 amri ya kwanza ya kutotoka nje ilitekelezwa tarehe 31 mjini Washington DC.

    CNN pia imesema hivi sasa wananchi wa Marekani wanasubiri rais Trump atoe hotuba kuhusu maandamano yaliyotokana na mauaji ya George Floyd.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako