• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema reli ya SGR iliyojengwa na China itaweza kustawisha miji na kufungua masoko mapya

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:47:05

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema reli ya SGR iliyojengwa na China ambayo ilirefushwa kwa kilomita 485 kutoka Mombasa hadi Naivasha, itahimiza ukuaji wa miji nchini humo na kufungua masoko mapya barani Afrika.

    Rais Kenyatta amesema hayo katika maadhimisho ya miaka 57 ya uhuru, huku akiongeza kuwa wakosoaji dhidi ya reli ya SGR wakiwa kama waliokosoa reli kongwe iliyojengwa mwaka 1901 watathibitishwa kuwa wamekosea.

    Amesema reli ya SGR ndio ukosoaji mkubwa dhidi yake, lakini wakosoaji hao hawako peke yao, wako pamoja na wakoloni walioita reli iliyojengwa wakati wa ukoloni kama "reli ya wenda wazimu".

    Rais huyo akizungumzia mji mkuu ambao ukuaji wake ulichangiwa kwa kiasi na reli hiyo, amesema wale walioikosoa reli hiyo inayoelekea mahali pasipofahamika, bado hawajafahamu kuwa sehemu waliyoitaja wakati ule ni Nairobi, ambayo ilikuwa mahali pasipofahamika wakati reli hiyo ilipokuwa inajengwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako