• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya matibabu ya China yabadilishana uzoefu wa kupambana na COVID-19 na kamati ya dharura ya afya nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:47:57

    Timu ya matibabu ya China ambayo iko ziarani nchini Sudan, jana ilikutana na wajumbe wa Kamati kuu ya Dharura ya Afya nchini humo ili kubadilishana nao uzoefu wa mapambano dhidi ya COVID-19.

    Mjumbe wa kamati hiyo Bw. Hiba Ahmed kwenye taarifa amesema, timu ya matibabu ya China imefanya ziara nchini Sudan ili kujua hali ya kiafya na changamoto zinazoikabili Sudan kwenye mapambano dhidi ya COVID-19.

    Wakati huo huo Balozi wa China nchini Sudan Bw. Ma Xinmin, amesisitiza kuwa, ushirikiano kati ya China na Sudan kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona unaendelea.

    Balozi Ma amesema China inafanya juhudi kuiunga mkono Sudan kwa njia inayofaa zaidi, ambayo ni kubadilishana uzoefu kuhusu kusimamia na kudhibiti COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako