• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yapata shehena ya tatu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Jack Ma

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:48:22

    Sudan Kusini imepata shehena ya tatu ya vifaa tiba vilivyochangiwa na Mfuko wa Jack Ma na Alibaba kwa ajili ya kupambana na COVID-19.

    Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Hua Ning, amesema vifaa hivyo ni pamoja na barakoa milioni 4.6, vitendanishi laki 5, mashine 300 za kupumulia, nguo za kujikinga laki 2, kofia za kujikinga laki 2, vipima joto 2,000, na jozi 500,000 za glavu.

    Balozi Hua amesema mchango huo kwa Sudan Kusini umesambazwa na Umoja wa Afrika.

    Hadi kufikia tarehe 27 mwezi Mei, Sudan Kusini ilikuwa imeripoti maambukizi 994 ya COVID-19, watu 6 wamepona na wengine 10 wamekufa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako