• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko mpya wa virusi vya Ebola waripotiwa kaskazini magharibi mwa DRC

    (GMT+08:00) 2020-06-02 10:01:37

    Mlipuko mpya wa virusi vya Ebola umetangazwa na waziri wa afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Bw. Eteni Longondo katika mji wa Mbandaka, mkoa wa Ikweta kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

    Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Bw. Longondo amesema sampuli zilizochukuliwa Mbandaka na kupelekwa kwenye Taasisi ya Utafiti wa kibioloji ya taifa mjini Kinshasa, zimeonyesha kuwa watu hao wameambukizwa, na timu ya mwitikio wa Ebola iko tayari katika ngazi ya mkoa na timu nyingine itapelekwa kutoka Kinshasa ili kuimarisha mwitikio dhidi ya janga hilo.

    Mkurugenzi mkuu wa WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amethibitisha kuwa watu sita wameambukizwa, na wengine wanne wamekufa. Amesema shirika hilo liko tayari kutuma timu zake kuisaidia nchi hiyo kupambana na mlipuko huo wa Ebola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako