• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la nchini Nigeria lalaani vizuizi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-02 18:42:24

    Gazeti la This Day la nchini Nigeria limesema, watu weusi nchini Marekani wanashindwa kufikia uwezo wao kikamilifu kutokana na vizuizi vilivyowekwa na wazungu.

    Maoni yaliyochapishwa na gazeti hilo chini ya kichwa "Kifo Kisicho na Sababu cha George Floyd" yalikuwa na maswali kadhaa, ikiwemo sababu ya watu weusi kulengwa katika mauaji ya hivyo na askari wa kizungu, na nini kimetokea katika ujumuishi na umoja.

    Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd aliuawa baada ya polisi wa kizungu kumkandamiza shingioni kwa goti lake kwa dakika 8 mpaka alipoacha kupumua. Tukio hilo limezusha maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani, na kulazimisha marufuku ya kutembea usiku kutolewa katika maeneo kadhaa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako