• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu karibu milioni 10 mjini Wuhan wafanyiwa upimaji wa virusi vya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-02 19:10:52

    Wakazi milioni 9,899,828 mjini Wuhan mkoani Hubei wamepimwa virusi vya Corona (COVID-19) kuanzia tarehe 14 mwezi Mei hadi tarehe 1 mwezi Juni.

    Mtaalamu wa taasisi ya matibabu ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Huazhong Bw. Lu Zuxun amesema, hakuna mtu yeyote aliyegunduliwa kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo katika vipimo hivyo.

    Wakati huo huo, vipimo hivyo viligundua watu 300 wenye virusi wasioonyesha dalili, na pia watu 1,174 waliwasiliana kwa karibu na wagonjwa walifuatiliwa na majibu yao ya vipimo yalionyesha hawajaambukizwa.

    Kamati ya afya ya mji wa Wuhan imesema, vipimo hivyo vinatolewa bure na kwa hiari, huku gharama zote zikilipwa na serikali za mji na za mitaa. Kaimu Meya ya mji wa Wuhan Hu Yabo amesema, mji huo ulitumia jumla ya dola za kimarekani milioni 126 ili kufanikisha vipimo kwa wakazi wa mji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako