• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatuma watalaamu 148 kwa nchi 11 za Afrika kwa kuzisaidia kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-02 19:11:14

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo hapa Beijing amesema, China imetuma vikundi 148 vya wataalam wa matibabu kwa nchi 11 za Afrika ili kuzisaidia nchi hizo kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Bw. Zhao Lijian amesema, wataalamu wa China walifanya mawasiliano na idara husika na madaktari wa nchi za Afrika na kubadilishana nao uzoefu wa kupambana na COVID-19.

    Kuhusu hali ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Afrika, Bw. Zhao amesema, mradi huo ni mafanikio muhimu ya mkutano wa kilele wa Beijing wa mwaka 2018 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, pia ni hatua muhimu ya China kuisaidia Afrika kuimarisha mfumo wao wa kukinga na kudhibiti magonjwa na ujenzi wa uwezo wa afya ya jamii. Amesema China itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na Afrika katika sekta ya matibabu na afya kutokana na maendeleo ya hali ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako