• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi wanne wa Sudan Kusini wauawa kwa risasi na wenzao wa Uganda kwenye eneo la mpaka lenye utata

    (GMT+08:00) 2020-06-02 19:18:56

    Askari wanne wa Sudan Kusini wameuawa na mmoja kujeruhiwa baada ya wanajeshi wa Uganda kuwafyatulia risasi huko Buya jumapili iliyopita.

    Msemaji wa jeshi la ulinzi la Sudan Kusini Lul Ruia Koang ameliambia shirika la habari la China Xinhua kuwa, tukio hilo kati ya majeshi ya nchi hizo lilitokea baada ya pande hizo kurushiana risasi katika eneo lenye utata, lililipo kusini mwa Sudan Kusini.

    Eneo hilo linagombewa na jamii za kaunti ya Kajo-Keji, jimbo la Ikweta ya Kati nchini Sudan Kusini na majirani zao kutoka wilaya ya Yumbe nchini Uganda.

    Hali kwa sasa imekuwa tulivu katika eneo hilo baada ya serikali za nchi hizo mbili kukubaliana kuchunguza chanzo cha pambano hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako