• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KENYA WAKULIMA wa mahindi katika eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa wanatarajiwa kupata afueni kufuatia kukamilishwa kwa ujenzi wa kiwanda cha kusaga unga wa mahindi.

    (GMT+08:00) 2020-06-02 19:49:36

    Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Moi-Soy, Belfast Sang, amesema kuwa kiwanda hicho kimejengwa kwa ushirikiano na serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu kwa kima cha Sh477 milioni.

    Amesema kuwa sababu ya kujenga kiwanda chao ni kujikinga na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakinunua mahindi yao kwa bei duni.

    Kulingana na waziri wa Vyama vya Ushirika na Biashara wa Kaunti ya Nandi Esther Mutai, serikali ya kaunti imechangia Sh230 milioni katika ujenzi wa mradi huo. Wanachama wa chama hicho cha ushirika walichangia jumla ya Sh247 milioni.

    Serikali ya kaunti inaamini kuwa kiwanda hicho kitakinga wakulima dhidi ya ushindani mkali ambao husababishwa na mahindi yanayofurika humu nchini kutoka katika mataifa jirani

    Serikali ya kaunti imesema kuwa mradi huo utanufaisha wakulima wote kutoka katika eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa ambalo huzalisha chakula kinachotumiwa katika maeneo mengi ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako