• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yakanusha kuingilia mambo ya ndani ya Marekani kufuatia ghasia zinazoendelea nchini humo dhidi ya ubaguzi wa rangi

    (GMT+08:00) 2020-06-02 20:06:05
    Waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa wa Zimbabwe Sibusiso Moyo ametoa taarifa akipinga kauli iliyotolewa na naibu msaidizi wa usalama wa taifa wa Marekani Robert O'Brien kuwa nchi hiyo inaingilia kati mambo ya ndani ya Marekani kwa kutumia maandamano yanayoendelea nchini humo dhidi ya ubaguzi wa rangi.

    Bw. Moyo amesema serikali ya Zimbabwe jana ilimwita balozi wa Marekani Brian Nichols kufuatia kauli hiyo, na kumwarifu kuwa shutuma hizo ni za makosa na hazina msingi wowote, na zitaharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Siku ya Jumapili, naibu msaidizi wa usalama wa taifa wa Marekani Robert O'Brien alisema maandamano hayo yalichochewa na nchi za nje ikiwemo Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako