• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Prof Humphrey Moshi wa Tanzania aunga mkono uamuzi wa bunge la umma la China kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa Hongkong

    (GMT+08:00) 2020-06-03 08:46:12

    Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa China katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania Prof Humphrey Moshi, ameunga mkono uamuzi wa bunge la umma la China kupitisha sheria ya usalama wa taifa kwa mkoa wa Hong Kong.

    Akihojiwa na wanahabari wa Shirika la Habari la China Xinhua na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Profesa Moshi amesema mfumo wa sheria wa usalama wa taifa ni msingi wa nchi na sehemu zote kulinda uendeshaji wa kawaida wa siasa, uchumi na jamii. Shughuli za kimabavu na ufarakanishaji zilizotokea huko Hong Kong zinaonyesha kuwa mchakato wa kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong umechelewa, ukosefu wa sheria ya kulinda usalama wa taifa ulitoa fursa kwa makundi mbalimbali ya ndani na nje kuingilia kiharamu mambo ya Hong Kong na kuvuruga usalama wa taifa wa China.

    Amesema uamuzi wa bunge la umma la China wa kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong umetolewa kwa wakati, ni wa lazima, na utatoa uhakikisho katika kuzuia Hong Kong kukumbwa tena na fujo na kulinda ukamilifu wa sera ya "nchi moja, mifumo miwili".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako