• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wasema Marekani haina mamlaka ya kubadilisha nchi wanachama wa G7 wala kubadili taratibu za mikutano

    (GMT+08:00) 2020-06-03 09:04:15

    Baada ya rais Donald Trump wa Marekani kuahirisha mkutano wa kilele kuhusu upanuzi wa Kundi la Nchi Saba G7, ofisa mkuu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bw. Josep Borrell Fontelles, amesema Marekani ikiwa ni mwenyekiti wa zamu wa G7, haina mamlaka ya kubadilisha nchi wanachama wa G7 wala kubadili taratibu za mikutano ya kundi hilo.

    Kutokana na mpango wa rais Trump uliotolewa tarehe 30 mwezi Mei, Marekani inapanga kuzialika Russia, Korea Kusini, Australia na India kuhudhuria mkutano huo. Kuhusu hilo Bw. Borrell amesisitiza kuwa Umoja wa Ulaya bado unapinga Russia kurudishwa tena kwenye kundi la G7 baada ya nchi hiyo kuondoka mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako