• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Putin aidhinisha sera ya kimsingi ya Russia kuhusu kuzuia mashambulizi ya kinyuklia

    (GMT+08:00) 2020-06-03 10:07:08

    Rais Vladimir Putin wa Russia amesaini amri ya kuidhinisha sera ya kimsingi ya Russia juu ya kuzuia mashambulizi ya kinyuklia, ambayo imeanza kufanya kazi tangu itangazwe jana.

    Kituo cha taarifa ya kisheria cha Russia kimetangaza waraka husika uliosainiwa na rais Putin. Waraka huo umesema Russia inachukulia silaha za kinyuklia kama mbinu ya kutishia maadui, ambazo zitaruhusiwa kutumika katika hali ya kulazimika. Russia itachukua hatua zote za lazima katika kupunguza tishio linalotokana na silaha za kinyuklia, ili kuzuia kutokea kwa mapambano ikiwa ni pamoja na mapambano ya kinyuklia kutokana na mivutano ya kimataifa.

    Waraka huo umeongeza kuwa sera hiyo ya kiulinzi inalenga kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, na kutishia maadui wa Russia ili kuwazuia kufanya uvamizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako