• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Janga la COVID-19 litaweza kuwafanya watu milioni 60 kukumbwa na umaskini uliokithiri

    (GMT+08:00) 2020-06-03 10:13:01

    Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw. David Malpass, amesema uchumi wa dunia unakumbwa na pigo kubwa kutokana na janga la COVID-19 ambalo mwaka huu litaweza kuwafanya watu zaidi ya milioni 60 kuangukia katika umaskini uliokithiri.

    Kwenye ripoti ya Matarajio ya Uchumi wa Dunia, Bw. Malpass amesema nchi zinazoendelea zinakabiliwa na tishio lisilotarajiwa la kiafya na kiuchumi, ambalo litaathiri maendeleo kwa miongo kadhaa.

    Ripoti hiyo pia inasema hatua kali za karantini zilizochukuliwa kukabiliana na janga hilo la COVID-19 zimesababisha kudorora kwa uchumi katika nchi mbalimbali.

    Bw. Malpass pia amesisitiza kuwa ili kukabiliana na janga hilo, Benki ya Dunia itafanya juhudi za kupunguza hasara na kuzisaidia nchi mbalimbali kufufuka ili kufanya ukarabati na kuwa na nguvu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako