• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klabu Ligi Kuu Zanzibar zamjadili rais wa ZFF

    (GMT+08:00) 2020-06-03 16:35:54

    Umoja wa Klabu za Ligi Kuu Zanzibar umekutana jana na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) kwa lengo la kujadili kiini cha kutokuwepo na maelewano na rais wa ZFF, Seif Kombo Pandu. Mwenyekiti wa kikao hicho Haji Kidali amesema, kikao hicho maalum kiliandaliwa na viongozi wa Umoja wa Klabu Zanzibar, kwa lengo la kutaka kujua kiini cha baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuandika barua ya kutokuwa na imani na rais wa ZFF, wakati kama kuna tatizo wangeweza kutumia njia ya kukutana na Umoja huo waliouchagua wao wenyewe. Lakini ameeleza matumaini yake kuwa wanaweza kufikia muafaka wa kumaliza sintofahamu iliyojitokea kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako