• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Morrison, Tshishimbi waitia hofu Yanga

    (GMT+08:00) 2020-06-03 16:37:33

    Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji nyota wa timu hiyo, winga mshambuliaji Bernard Morrison na kiungo mkabaji Papy Tshishimbi wameitia hofu timu hiyo baada ya kupata majeraha, na wanaendelea kuwafuatilia kwa karibu. Amesema majeraha yao si makubwa, lakini ana imani kuwa mpaka kufikia Juni 13 watakuwa wako vizuri kusafiri na timu kuelekea Shinyanga kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Mwadui FC. Ameongeza kuwa wamejipanga vizuri kuelekea mchezo huo licha ya kwamba wanatambua kuwa kucheza ugenini kuna changamoto zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako