• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kai Havertz amnyima usingizi Solskjaer

    (GMT+08:00) 2020-06-03 16:51:06

    Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameripotiwa kuongoza harakati za kumnasa kiungo mshambuliaji wa Bayer 04 Leverkusen ya Ujerumani, Kai Havertz. Solskjaer anaamini kiungo huyo atatosha kuleta mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kuanzia msimu ujao, endapo atafanikiwa kumsajili wakati wa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi. Meneja huyo kutoka nchini Norway pia amedhamiria kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, ambaye mwishoni mwa juma lililopita alipiga hat-trick wakati timu yake ilipoichapa Paderborn 6-1 kwenye ligi ya Bundesliga. Hata hivyo mpango namba moja wa Solskjaer ni kumsajili Sancho, lakini baada ya hapo atajizatiti kumnasa Havertz, ambaye anaamini asipofanya hivyo kwa mwaka huu, huenda thamani yake ikuwa kubwa zaidi mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako