• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xinjiang yakanusha kuwakataza waislamu kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani

    (GMT+08:00) 2020-06-03 17:15:34

    Mkurugenzi wa kamati ya masuala ya kikabila ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur Bw. Mekhmut Usman amewalaumu wafuasi wa kundi la Turkistan Mashariki lililopo nje ya China kwa kusema mkoa huo uliwakataza waislamu kufunga katika mwezi wa Ramadhani, na kusisitiza kuwa shughuli za kidini katika mwezi huo mtufuku ziliendelea vizuri.

    Bw. Usman amesema kila inapofika mwezi wa Ramadhani, wafuasi hao wanasambaza uwongo kama huo kwa nia ya kudhuru uhusiano wa kikabila, kuharibu umoja wa kitaifa, na kuchochea chuki za kikabila. Amesema Xinjiang inatekeleza ipasavyo sera ya taifa ya kulinda uhuru wa kuabudu, watu wenye imani na wasio na imani wanapewa haki sawa katika sekta za siasa, uchumi, jamii na utamaduni, na watu wana uhuru wa kuchagua dini ya kuabudu. Ameongeza kuwa kundi ama mtu yeyote haruhusiwi kuzuia makundi ya kidini au watu binafsi kushiriki kwenye shughuli halali za kidini kwa mujibu wa sheria.

    Kuhusu shutuma zilizotolewa na wafuasi wa kundi la Turkistan Mashariki kuwa mlipuko wa virusi vya Corona ulitokea katika vituo vya kutoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi mkoani Xinjiang, mkurugenzi wa kamati ya afya na matibabu ya mkoa huo Mutarif Rozi amesema, wakufunzi wote wa vituo hivyo walihitimu mwezi Disemba mwaka jana, hivyo si kweli kwamba mlipuko ulitokea katika vituo hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako