• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika na nchi nyingi za Afrika zalaani mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya kiafrika nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:36:02

    Tukio la mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd yaliyofanywa na polisi mzungu wa jimbo la Minnesota, Marekani limesababisha vurugu kubwa nchini humo. Kitendo cha matumizi ya mabavu na ubaguzi nchini Marekani kimelaaniwa kwa pamoja na Umoja wa Afrika na nchi za Afrika……………

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat ametoa taarifa akisema, Umoja huo umelaani mauaji hayo, na kamwe hautakubali ubaguzi wa rangi nchini Marekani dhidi ya wamarekani wenye asili ya Afrika. Pia Bw. Faki ameitaka serikali ya Marekani kuongeza juhudi kuhakikisha inaondoa aina zote za ubaguzi kwa msingi wa rangi ama kabila.

    Rais wa Ghana Nana Akuffo-Addo amesema, tukio hilo limeleta hisia mbaya iliyowahi kutokea zamani, pia ni onyo kwa watu wote. Amesema watu weusi, duniani kote, wameshtushwa na kusikitishwa na mauaji ya mtu ambaye hakuwa na silaha yaliyofanywa na askari polisi wa kizungu, limeamsha kumbukumbu mbaya kwa watu weusi. Amesema wako pamoja na ndugu zao Wamarekani weusi katika wakati huu mgumu, na kutarajia kuwa kifo cha George Floyd kitaleta mabadiliko ya kudumu kuhusu jinsi Marekani inakabiliana na matatizo ya chuki na ubaguzi wa rangi.

    Chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC pia kimetoa taarifa kuwa, kiwango cha dharau cha Marekani kwa maisha ya watu weusi kimekuwa hatari sana, ambapo matukio ya kimabavu yanayosababisha vifo vya watu weusi yameleta wasiwasi. Ingawa Marekani imeondoa ubaguzi wa rangi kwa miaka karibu 70, lakini hivi sasa watu wasio wazungu bado walishambuliwa kutokana na tofauti ya rangi.

    Mauaji ya George Floyd yamesababisha maamdamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi na matumizi mabaya ya nguvu yanayofanywa na polisi nchini Marekani, na kuwafanya mameya na magavana wa majimbo yote nchini humo kuweka vizuizi vya kutembea usiku katika zaidi ya miji 40, huku maelfu ya watu wakishikiliwa na polisi.

    Kufuatia hilo, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, katibu mkuu huyo Antonio Guterres ametoa wito kwa mamlaka zinazokabiliana na waandamanaji nchini Marekani kujizuia, na kuongeza kuwa anatarajia kuona maandamano ya Amani nchini humo kufuatia kifo cha Floyd.

    Kama ambavyo nchi za Afrika zimelaani mauaji hayo, nchi za Ulaya pia zimepinga kitendo hicho cha kikatili, ambapo nchini Canada, waandamanaji walivamia mitaa ya Montreal kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili unaofanywa na jeshi la polisi.

    Mamia ya wafuasi wa tawi la vijana la Chama cha KKE nchini Ugiriki nao waliandamana kwa Amani nje ya jengo la ubalozi wa Marekani mjini Athens na ubalozi mdogo wa Marekani ulioko kwenye mji wa kaskazini wa Thessaloniki. Waandamaji hao walikuwa na mabango yaliyoandikwa "Siwezi kupumua", wakisema wanaungana na wenzao wa Marekani ambao kila siku wanahangaika kutafuta haki zao, wawe na uwezo wa kupumua.

    Nchini Uingereza, maelfu ya watu walikusanyika jijini London na Manchester walipinga mauaji ya Floyd, licha ya serikali ya nchi hiyo kuzuia mikusanyiko ya watu.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Heiko Maas amesema, maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani yanaeleweka na ni halali. Naye Ofisa mkurugenzi wa masuala ya sera za kidiplomasia na usalama katika Umoja wa Ulaya a Bw. Josep Borrell ameeleza tukio hilo kama matumizi mabaya ya madaraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako