• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika ya Mashariki zaunga mkono kanuni ya kuwepo kwa China moja na sera ya Nchi moja, Mifumo miwili

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:40:38

    Nchi za Afrika Mashariki zimeeleza kuunga mkono hatua ya China ya kutunga sheria ya kujenga na kukamilisha mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa Mkoa wenye Utawala Maalum wa Hong Kong, na kusema mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, na nchi nyingine hazina haki ya kuingilia kati mambo hayo.

    Msemaji wa serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas amesema, serikali ya Tanzania inaunga mkono sera ya Nchi Moja, Mifumo Miwili, na kupinga nchi za nje kuingilia kati ya mambo ya Hong Kong. Amesema utungaji wa sheria ya kulinda usalama wa taifa wa mkoa wa Hong Kong ni hatua muhimu ya Bunge la Umma la China kwa kulinda usalama wa taifa la China, kurudisha utaratibu wa utekelezaji wa sheria na kulinda maisha ya kawaida ya wakazi wa Hong Kong.

    Serikali ya Burundi nayo imeeleza kuunga mkono uamuzi huo wa Bunge la Umma la China, ikisema uamuzi huo utasaidia kulinda utekelezaji wa sheria na kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya China.

    Msemaji wa serikali ya Uganda Bw. Ofwono Opondo amesema, Hong Kong ni sehemu isiyotengeka ya China, na mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, hivyo njama za nchi za magharibi za kuitenganisha China hazitafanikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako