• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yapanga kutoza kodi ya thamani huduma za dijitali

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:41:27

    Serikali ya Kenya inapanga kuanza kutoza kodi ya thamani kwa huduma za Uber, Netflix na nyingine za runinga na burudani.

    Hii ni baada ya wizara ya fedha kuchapisha rasimu ya sheria ya mwaka 2020 ya kukusanya ushuru kutoka kwa huduma za kidijitali.

    Biashara zingine zinazolengwa ni pamoja na uuzaji wa tikiti za elektroniki na programu za kompyuta.

    Watumiaji wa huduma hizo wanatarajiwa kulipia gharama mpya za ushuru na wauzaji nao watahitajika kuwasilisha kumbukumbu za mauzo na ushuru waliolipa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako