• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Home Africa imetangaza hasara ya dola milioni 8.4

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:42:11

    Kampuni ya ujenzi wa nyumba nchini Kenya Home Africa imetangaza hasara ya dola milioni 8.4 kwa mwaka uliomalizika Desemba 2019.

    Mwaka jana, kampuni hiyo iliripoti hasara ya dola milioni 3.4

    Mkurugenzi Mtendaji wake Dan Awendo amesema hasara hiyo imechangiwa na kupanda kwa bei ya ardhi.

    Hasara hiyo imetokea licha ya kampuni hiyo kuwa na ukuaji wa asilimia 233 katika mapato ya jumla - kutoka dola milioni 1 hadi dola milioni 3.6 mwaka 2019.

    Bwana Awendo amesema mauzo halisi ya Home Africa yalikua kutoka dola milioni 5.8 mwaka 2018 hadi dola milioni 6.4 mwaka 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako