• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar: Majengo kale kuvutia watalii

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:43:12

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imejipanga kuimarisha na kutangaza utalii wa majengo ya kale kwa lengo la kuwawezesha watalii wanaokuja kujuwa historia ya makumbusho na watawala waliotawala Zanzibar.

    Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo, katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akielezea juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Oman, kuimarisha mambo ya kale ikiwamo majengo ya historia na nyaraka.

    Alisema Serikali ya Oman ndiyo iliyochukua jukumu la kuimarisha majengo ya historia pamoja na nyaraka za makumbusho ambayo ndiyo zinazoweza kubeba utalii wa Zanzibar na kuwawezesha wasomi na mabingwa wa fani mbalimbali kuja nchini na kusoma historia hiyo.

    Alisema nyumba ya nyaraka iliyopo Kilimani imepatiwa mitambo ya kuhifadhi nyaraka pamoja na kuwekwa vifaa ambavyo vitasaidia kuimarisha uhai wa nyaraka hizo na kuwa bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako