• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: watanzania watakiwa kujinufaisha na soko la ndani la mafuta

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:43:31

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki, ametaka Watanzania kuwekeza katika sekta ya mafuta ya kula kutokana na kuwapo kwa soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

    Aliyasema hayo wakati akikagua kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula cha Sunshine kinachozalisha mafuta yanayotengenezwa kwa kutumia malighafi ya alizeti yanayoitwa Sunbelt kilichoko katika eneo la Zuzu.

    Waziri huyo alibainisha kuwa uwekezaji huo ni miongoni mwa fursa muhimu na kuwataka wenye uwezo kulima zao hilo kwa wingi, kuchangamkia fursa hiyo kwa vile zao hilo linastawi katika ukanda wa Dodoma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako