• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ghasia ya maandamano nchini Marekani yasababisha vifo vya watu 11 na wengi ni wenye asili ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:44:49

    Kituo cha Televisheni cha Los Angeles nchini Marekani kimesema, maandamano ya kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 11, wengi wakiwa ni Wamarekani wenye asili ya Afrika na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, ingawa idadi kamili haijahesabiwa.

    Habari nyingine zinasema, watu karibu 4,400 nchini Marekani wamekamatwa kutokana na maandamano hayo kwa makosa ya uporaji, kukiuka amri ya kutotoka nje wakati wa usiku na kufunga barabara. Miji 40 za Marekani ikiwemo Washinton, Los Angeles na New York imeanza kutekeleza sera ya kutoruhusu kwenda nje wakati wa usiku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako