• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Uingereza iepuke kuingia hatarini kufuatia kauli yake kuhusu Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-06-03 19:13:32

    China imeitaka Uingereza iepuke kuingia hatarini kutokana na kauli zake kuhusu utungaji sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong, na kutambua na kuheshimu ipasavyo hali halisi kuwa Hong Kong ni sehemu ya China na kuwa eneo lenye utawala maalumu nchini humo.

    Kauli hiyo ya China imekuja baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Dominic Raab kusema hatua ya China kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong inaharibu sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", na ni kinyume na wajibu wa kimataifa wa China. Pia ametoa tahadhari kuwa kama China inaharibu msingi wa siasa na kujitawala kwa Hong Kong, itaweza kutishia muundo wa uchumi na ustawi wa eneo hilo kwa muda mrefu.

    Akizungumzia kauli hizo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema ni wajibu kwa serikali ya China kutunga sheria ya ulinzi wa taifa katika Hong Kong, na baada ya Hong Kong kurudi China, Uingereza haina mamlaka wala haki ya kutawala na kuongoza Hong Kong, na haitakiwi kutoa maoni juu ya masuala ya Hong Kong na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

    Bw. Zhao amesisitiza kuwa sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" inaweza kulindwa iwapo usalama wa taifa unalindwa, na kisha ustawi na utulivu wa Hong Kong unaweza kulindwa. Amesema utungaji sheria hiyo unalenga vitendo vya kuharibu usalama wa taifa la China vinavyofanywa na watu wachache, na hauathiri Hong Kong kujitawala kwa kiwango cha juu, hauathiri haki na uhuru wa wakazi wa Hong Kong, wala hauathiri maslahi halali ya wawekezaji wa kigeni katika Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako