• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNECA: Mlipuko wa COVID-19 wakadiriwa kuwafanya waafrika milioni 29 kuangukia katika ufukara

    (GMT+08:00) 2020-06-04 08:58:33

    Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA imekadiria kuwa mlipuko unaoendelea wa virusi vya Corona utawafanya watu milioni 29 kuangukia katika umaskini uliokithiri kote barani Afrika.

    UNECA imesema kupitia taarifa kuwa, Afrika inashuhudia athari za kiuchumi zinazotokana na janga la COVID-19, hata kabla ya athari zake kwa afya ya umma. Imeongeza kuwa Ukuaji wa uchumi wa Afrika unakadiriwa kupungua kwa asilimia 1.8 hadi asilimia 2.6, hali ambayo itakuwa na athari hasi kwa juhudi za kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs katika bara hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako