• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi Kuu England inaporejea watu 300 tu ndio wataingia uwanjani

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:00:03

    Watu 300 tu ndio wataruhusiwa kuwa uwanjani wakati wa Ligi Kuu England itarejea. Hii itajumuisha idadi ya wachezaji, benchi la ufundi, wauguzi na madaktari lakini pia baadhi ya viongozi. Pamoja na hivyo, wahusika kadhaa watakaokuwa uwanjani na idadi ya mwisho inatakiwa watu wasizidi 300. Ligi Kuu England inatarajiwa kurejea Juni 17 kwa mechi za viporo na sababu kubwa ya kufanya hivi ni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona. Vifaa vyote vya michezo ikiwa ni pamoja na mipira, bendera vitapuliziwa dawa maalumu kwa ajili ya kinga zaidi. Mpango mkubwa uliopo kwa sasa uliopo na kila timu imetaarifiwa ni kuhusu utaratibu uliopangwa ni pamoja na mikutano ya waandishi wa habari kufanyika kupitia video call kipindi ligi itakaporejea. Watu wa VAR watakaa vyumba tofauti ili kuweka umbali kujikinga dhidi ya Virusi vya Corona. Wachezaji 20 kwa timu moja, dawati la madaktari na benchi la ufundi 12, viongozi kutoka kila timu 10. Hakutakuwa na mashabiki ndani ya Uwanja zaidi ya watu 300 ambao wana majukumu maalumu ya kufanya. Watu wa uzalishaji matangazo hawatazidi 23 kwa upande wa waandishi watahitajika 60.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako