• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa yakubali kumkabidhi mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda kwenye mahakama ya Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:21:49

    Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeripoti kuwa Ufaransa imekubali kumkabidhi mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda Felicien Kabuga kwenye mahakama ya Umoja wa Mataifa.

    Habari zinasema Bw. Kabuga alikamatwa kwenye kitongoji cha Paris tarehe 16 Mei. Aliwahi kutoa msaada wa fedha kwa mauaji makubwa yaliyotokea kati ya mwezi Aprili hadi Juni mwaka 1994 nchini Rwanda, tukio ambalo lilisababisha vifo vya watu laki nane. Bw. Kabuga alikimbilia na kuishi Uswisi, Zaire na Kenya, kwa zaidi ya miaka 20.

    Bw. Kabuga ambaye ni mmoja wa wahalifu waliokuwa wanasakwa duniani, akiwa mhalifu mkubwa wa mauaji ya halaiki katika historia ya binadamu, alihukumiwa uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari. Serikali ya Marekani ilitoa amri ya kumsaka kwa donge nono la dola za kimarekani milioni tano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako