• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa ulinzi wa Marekani hakubali kutuma jeshi kuondoa fujo nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:22:13

    Gazeti la Capital Hill la Marekani limeripoti kuwa, waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Bw. Mark Esper amesema hakubali kutekeleza Sheria ya Uasi ambayo itamruhusu rais Trump kutuma jeshi kutawanya maandamano yanayoendelea kote nchini humo.

    Bw. Esper amesema anaamini kutokana na hali ilivyo sasa, kikosi cha polisi kinafaa zaidi kutekeleza sheria nchini humo, na jeshi linatakiwa kutumwa kama hatua ya mwisho katika hali ya hatari na dharura, na hivi sasa bado hakuna hali kama hii.

    Rais Trump wa Marekani jana alitoa hotuba yenye msimamo mkali akidai kuwa sauti ya waandamanaji wa amani haiwezi kuzimwa na "majambazi", na kwamba atatuma askari, wanajeshi na maofisa wa utekelezaji wa sheria kuondoa fujo. Kauli yake hii imepingwa na kukosolewa na pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako