• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika apinga ubaguzi wa rangi na hali ya kukosa uvumilivu kuhusu kifo cha Floyd

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:28:07

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, amezitaka nchi mbalimbali duniani ziepuke ubaguzi wa rangi na hali ya kukosa uvumilivu.

    Rais Ramaphosa amesema hayo aliposhiriki kwenye mkutano maalumu wa kilele wa kwanza wa nchi za Jumuiya ya Afrika, Caribbean and Pasifiki uliofanyika kwa njia ya video.

    Rais Ramaphosa amesema Umoja wa Afrika unalaani vikali mauaji ya George Floyd nchini Marekani, na umekasirishwa kama mamilioni ya watu huko Marekani na duniani kote.

    Wakati huo huo rais Ramaphosa amesisitiza uungaji mkono kwa Shirika la afya duniani (WHO), ameongeza kuwa WHO imeonesha umuhimu mkubwa katika kuzisaidia nchi mbalimbali kupambana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako