• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Rwanda asisitiza umuhimu wa ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:28:33

    Rais Paul Kagame wa Rwanda ametoa mwito wa ushirikiano wa karibu na kutegemeana kwenye mapambano ya kimataifa dhidi ya COVID-19.

    Kwenye mkutano wa kilele wa kwanza wa nchi za Jumuiya ya Afrika, Caribbean na Pasifiki uliofanyika kwa njia ya video, rais Kagame amesema athari za COVID-19 zitaendelea kuwepo kwa muda mrefu baada ya virusi kushindwa, na njia ya kupona pia itakuwa ndefu sana. Kuimarisha ushirikiano na kutegemeana ni nyenzo kuu ya kuhakikisha nchi zote zinashirikishwa na sauti zote zinasikika.

    Amezitaka nchi za jumuiya hiyo ziimarishe ushirikiano kwenye kuzuia kuenea kwa janga hilo na kuongeza utulivu wa kiuchumi, na hasa zinatakiwa kuimarisha uratibu ili kuhakikisha zinapata matibabu, chanjo, na vifaa tiba kwa usawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako